​JE, NI PEP AU MOURIHNO KATIKA NAFASI YA NNE?

Si mara ya kwanza ama pili wanapokutana makocha hawa. Maswali ambayo yanaibuka ni kuwa nani kati yao atanyakua alama tatu dhidi ya mwenzake. Mji wa Manchester utashuhudia vilabu vyake viwili, Manchester City na Manchester United, vikikaragaza kandanda katika uwanja wa Eithad leo saa tano kasoro dakika kumi na tano. Tetesi ni kuwa wote wamehofia kukutana kwao na kuna mchezo wa akili ambao unaendelea baina yao. Mourihno kocha wa Manchester United amedai kuwa wachezaji wake mahiri wameumia na hawataweza kujumuishwa katika mchezo huo. Mchuano huu pia utabainisha mbivu na mbiji kati ya vilabu hivi kwani atakayefunga mwenzake na kujitwika alama tatu kitaweza kumaliza ligi mbele ya mwenzake. Tabiri nani atakayeshinda kwani mwamuzi ni wewe binafsi. Tafsiri hali ilivyo jipe alama kwa kuwa mpevu wa kandanda. Kila heri kwa timu zote mbili.
Je, ni lipi lisilona mwisho? Mashabiki wa kilabu ya kandanda ya Chelsea mate yawadondoka wakitegea kwa hamu na ghamu kushinda taji la ligi kuu ya kandanda Uingereza. Hii ni baada ya kuwabinkiza kilabu ya Southampton mabao 4-1 hapo jumanne ugani Stamford Bridge. Eden Hazard raiya wa ubelgiji alitia kimyani bao la kwanza mnamo dakika ya nane baada ya kuandaliwa pasi murwa kutoka kwa Diego Costa. Kukawa na mpishano mkubwa wa nguvu kwani  vilabu vyote vilihitaji kupata ushindi. Dakika kumi natano baadaye wageni walipata kusawazisha bao ile na ukawa sare ya bao moja kwa moja. Mwenye nguvu mpishe, kabla ya kipindi cha kwanza kufika tamati Cahill alipata kufunga bao la pili. Katika kipindi cha pili mambo hayakuwa mrama kwa Southampton kwani Diego Costa aliendeleza ushindi wao kwa kufunga mabao mengine mawili. Ushindi  umewaleta karibu sana katika kunyakua taji hilo la ligi kuu Uingereza.

 

Advertisements
Categories:

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s